SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA CPA.DKT.REGINALD ABRAHAM MENGI

Imewekwa: May 03, 2019


Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha CPA. Dkt. Reginald Abrahamu Mengi aliyekuwa mwanzilishi, mmiliki na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited na Mwenyekiti wa nne wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA (1985-2000).

CPA. Dkt. Reginald Abrahamu Mengi, atakumbukwa kwa uwezo na mchango wake mkubwa katika kuendeleza Taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi nchini.

NBAA ilimtumia sana kama mtaalam na mshauri katika kuendeleza taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi nchini na hakika alikuwa mstari wa mbele katika kuendeleza Taaluma hii.

Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti, Wafanyakazi na Wanachama wote wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, Tanzania tunatoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE

Imetolewa na,

CPA Pius A. Maneno

MKURUGENZI MTENDAJI