Majukumu ya kisheria
Kwa mamlaka ya sheria ya uanzishaji, [sheria ya wahasibu na wakaguzi (usajili) (sura ya 286 RE: 2002) kama ilivyoelezwa chini ya kifungu cha 4, Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA)
Ina mjukumu na mamlaka yafuatayo:
- Kuendeleza na kutoa fursa na nyenzo za kuchunguza, kufundisha, uhasibu, ukaguzi na masomo shirikishi;
- Kuendesha mitihani na kutoa diploma, vyeti na tuzo nyingine za Bodi katika uhasibu, ukaguzi na masomo shirikishi.
- Kudhamini, kupanga na kutoa nyenzo kwa ajili ya mikutano semina na majadiliano, na ushauri kuhusu mambo yanayohusu uhasibu na masomo shirikishi
- Kupanga kwa ajili ya uchapishaji na usambazaji wa jumla wa machapisho yaliyotokana na shughuli za bodi
- Kueleza viwango na miongozo ya uhasibu au ukaguzi kadiri inavyofaa na kuhakikisha utimizwaji wa viwango na miongozo kwa masomo husika.
- Kutunza rejesta ya wakaguzi, wahasibu, watunza vitabu na kampuni/mashirika yanayofanya kazi hizo.
- Kufikiria na kuamua maombi ya usajili na kufanya usajili wa wakaguzi, wahasibu, watunza vitabu na kampuni/mashirika yanayofanya kazi hizo.
- Kusimamia shughuli na mwenendo wa wakaguzi, wahasibu, watunza vitabu na kampuni/mashirika yanayofanya kazi hizo.
- Kutathimini sifa za uhasibu wa nje kwa ajili ya kusamehewa sehemu ya mitihani ya Bodi.
- Kutunga muundo wa uhasibu wa Taifa na mitaala ya mafunzo na kusimamia mitaala yote ya mafunzo ya uhasibu kwenye taasisi za mafunzo nchini kote inafuata muundo wa uhasibu wa Taifa
- Kutathimini sifa za uhasibu wa taasisi za ndani kwa ajili ya kusamehewa sehemu ya mitihani ya Bodi
- Kufanya majukumu mengine baada ya kushauriana na Waziri
Majukumu ya kisheria ya Bodi yaliyotajwa hapo juu yamefupishwa kama ifuatavyo:-
- Usajili
- Usimamizi
- Uendelezaji taaluma ya uhasibu
- Uwekaji Viwango
- Kufanya majukumu mengine baada ya kushauriana na Waziri