Ada ya mchango wa mwaka

Kwa, mujibu wa Sheria ndogo za NBAA, kila mtu aliyesajiliwa atalipa kwenye bodi ada ya mchango wa mwaka tarehe 1 ya Julai kila mwaka baada ya kupokea hati ya madai kutoka Bodi kwa ajili ya mailipo ya ada ya mchango wa mwaka iliyotumwa kwenye anwani yake ya mwisho iliyofahamika.

Mtu aliyesajiliwa au kampuni inayoshindwa kulipa kwa wakati ada ya mchango iliyoelezwa, atatakiwa kulipa zaidi baada ya kipindi cha msamaha cha miezi mitatu kupita, faini kama adhabu kwa utaratibu ufuatao:

  1. Baada ya miezi mitatu tangu tarehe ya kutakiwa kulipa ipite; adhabu ya faini ya asilimia 25 ya ada iliyotakiwa;
  2. Baada ya miezi sita, tangu tarehe ya kutakiwa kulipa, ipite adhabu ya faini ya asilimia 50 ya ada iliyotakiwa
  3. Baada ya miezi tisa tangu tarehe ya kutakiwa kulipa, ipite adhabu ya faini ya asilimia 75 ya ada iliyotakiwa; au
  4. Baada ya miezi kumi na mbili tangu tarehe ya kutakuwa kulipa, ipite adhabu ya silimia 100 ya ada iliyotakiwa.

Mtu anayeshindwa kulipa ada ya mchango iliyoelezwa kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia tarehe ya mwisho ya malipo, pamoja na malipo ya ada inayotakiwa, atafutiwa usajili na Bodi.

JEDWALI LA VIWANGO VYA ADA YA MCHANGO WA MWAKA KWA MTU MMOJA MMOJA

AT

TZS 30,000

GA

TZS 75,000

ACPA & FCPA

TZS 130,000

ACPA-PP & FCPA-PP

TZS 180,000

AP

TZS 50,000

TACPA

SAWA NA USD 700

TACPA-PP

SAWA NA USD 800

VIWANGO VYA ADA YA MCHANGO WA MWAKA KWA KAMPUNI

SMALL

TZS 400,000

MEDIUM

TZS 1,000,000

LARGE

TZS 3,000,000