Msamaha wa Taasisi

Katika kuratibu na kusimamia mafunzo ya taaluma ya uhasibu nchini. Bodi inatambua na kufuatilia masomo yoye ya uhasibu yanayotolewa. na taasisi za mafunzo zinazotambuliwa katika Jamhuri ya Muungano . Madhumuni makuu ya kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa wahitimu wanaochukua masomo ya uhasibu wamekamilisha ngazi inayotakiwa ya elimu na kujifunza inayotimiza kwa ufanisi matarajio ya sekta ya ajira na wataweza kufanya mitihani ya kitaalamu kwa urahisi.

Kila taasisi inayotambuliwa kutoa masomo inatakiwa kusoma Application Procedures na kujaza Exemption Application Form na kuwasilisha kwa Bodi. Msamaha unatolewa kwa masomo ya uhasibu, baada bodi kujiridhisha kwa taasisi imetimiza masharti yaliyoelezwa kwenye Exemption Policy inayotoa maelekezo katika kutimiza masharti ya msamaha yaliyowekwa na Bodi. Angalia Taasisi za hivi sasa za mafunzo ya uhasibu zilizopewa zimeoneshwa kwenye kila taasisi. Tafadhali bofya hapa.