Temporary Associate Certified Public Accountant ( TACPA )

“Mwanachama wa muda” maana yake ni mtu ambaye si raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, na mwenye sifa ya kusajiliwa na Bodi na ametimiza masharti yaliyoelezwa kwa ajili ya usajili huo.

Mgeni huyo ni lazima ajaze fomu ya maombi ya usajili wa Mhasibu /CPA-PP iliyopo kwenye tovuti na aambatishe vifuatavyo:-

  • Nakala zilizothibitishwa za vyeti husika vivivyotolewa na chombo cha uhasibu cha kitaalamu cheche hadhi sawa kilichopo nje ya Tanzania;
  • Jina na anwani vya mwajiri kuwa kama mdhamini;
  • Wahasibu wawili wataalamu waliosajiliwa na Bodi (AVPA au FCPA) kuwa kama wadhamini;
  • Uthibitisho wa ajira na mwajiri wa nchini,
  • Picha mbili za hivi karibuni za pasipoti za mwombaji
  • Uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi iliyoelezwa na isiyorudishwa
  • Kusaini ahadi kuwa baada ya usajili, mtu huyo atatimiza masharti ya Sheria, Sheria ndogo, kanuni na maelezo mengine yanayotumika, na kutotumia cheo au barua ya utambulisho kabla ya kusajiliwa au baada ya kukoma kuwa mwanachama aliyesajiliwa, na kuahidi kufuata kwa ukamilifu kanuni za maadili ya kazi zilizotolewa na Bodi

Bodi, baada ya kupitia na kuzingatia maombi, kwa mujibu wa kanuni hii, itampa mwombaji aliyefanikiwa cheti cha usajili wa muda kuwa Certified Public Accountant,au hutegemea hali itakavyokuwa, certifies public accountant in public practice.

Baada ya usajili kufanikiwa kwenye Bodi, mwanachama aliyesajiliwa kwa muda nje ya Afrika Mashariki ni lazima afanye na kufaulu mtihani wa kubasilishaji katika utozaji kodi wa nchini na sharia ya kampuni katika kipindi cha miaka miwili baada ya kusajiliwa na katika masharti mengine kadiri Bodi itakavyo amua kila baada ya muda.