Taratibu za mtihani

Jinsi ya kuomba kujiunga na mitihani

Ingia kwenye mfumo wa usajili wa wanachama na wanafunzi (MEMS) ulio kwenye mtandao wa Bodi na fuata maelekezo

Maandalizi ya kujisomea

Bodi inasajili na kusimamia taasisi za kuendesha masomo ya mapitio kwa watahiniwa wanaojiandaa kwa mitihani ya Bodi . Taasisi hizi zinajulikana kuwa watoa mafunzo.

Watahiniwa wanatakiwa kuhudhuria masomo ya mapitio kwa watoa mafunzo waliosajiliwa ili wajiandae vya kutosha kwa mitihani ya bodi. Watahiniwa wanashauriwa kuhudhuria marejeo ya masomo kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kufanya mitihani ya bodi.

Barua ya udahili wa mitihani

Bodi inatoa barua ya udahili wa mitihani kwa watahiniwa wenye sifa za kufanya mitihani katika muhula husika kabla ya kuanza kwa mitihani. Barua ya udahili inapatikana kwenye mfumo wa MEMS.

Uahirishwaji wa mitihani

katika kuahirisha mtihani mtahiniwa anatakiwa kufuata taratibu za uahirishwaji zilizoelekezwa.

Kukata rufaa

Kwa mtahiniwa anayetaka kukata rufaa, aingie kwenye mfumo wa wanachama na wanafunzi (MEMS) unaopatikana katika tovuti ya Bodi na kufuata maelekezo