Kuahirishwa kwa Mitihani

Kuahirishwa kwa Mitihani

Bodi hukubali kuahirishwa kwa mtihani kwenye matukio yafuatayo:-

1.Kuahirishwa ndani ya tarehe zinazokubalika

Mtahiniwa anayetaka kuahirisha mtihani anaweza kufanya hivyo kwa maandishi na anatakiwa apeleke maombi yake Bodi kabla ya tarehe 15 Februari kwa mitihani ya Mei na tarehe 15 Agosti kwa mitihani ya Novemba. Hapo, ada yote ya mtihani itapelekwa kwenye mtihani unaofuata. Mtahiniwa atatakiwa kujaza upya fomu ya kufanya mtihani kabla ya tarehe za kawaida za kufungwa kupokea fomu hizo.

2.Kuahirishwa baada ya tarehe zinazokubalika

Maombi ya kuahirishwa mitihani baada ya tarehe zinazokubalika yaani tarehe 15 Februari kwa mitihani ya Mei na tarehe 15 Agosti kwa mitihani ya Novemba huwa hayashauriwi sana. Kwenye tukio kama hili, mtahiniwa atatakiwa kulipa upya ada zote zinazohusika.

3.Kuahirishwa kunapokuwa na dharura

Panapotokea dharura, Bodi hukubali kupokea maombi ya kuahirishwa kwa mitihani ikiwa imeletwa na ushahidi.Mtahiniwa ambaye maombi yake ya kuahirisha mtihani yamekubaliwa na Bodi, atatakiwa kujaza upya fomu ya mtihani kwa kipindi cha mtihani kinachofuata na si baada ya hapo na kuipeleka kabla ya tarehe ya mwisho ya upokeaji wa maombi

Nusu ya ada inaweza kupelekwa kwenye mtihani unaofuatia kama maombi ya kufanya mtihani yamepelekwa ndani ya tarehe zinazokubalika.

Zingatia: Bodi itakubali kuahirishwa kwa mitihani kama mtahiniwa ataahirisha mitihani yote katika ngazi aliyosajili na si vinginevyo.