Kanuni za Mitihani

Kanuni za mitihani

1. Mtahiniwa ataruhusiwa kuingia kwneye ukumbi w amtihani angalau dakika 20 kabla ya kuanza kw amtihani, na hataruhusiwa kuondoka ukumbini mpaka baada ya dakika thelathini kumalizika . Vile vile watahiniwa hawataruhusiwa kuondoka kwenye ukumbi w amtihani dakika thelathini kabla ya mtihani kumalizika. Hakuna mtahiniwa atakayeruhusiwa kuingia katika chumba cha mtihani zaidi ya nusu saa baada ya kuanza kwa mtihani wowote. Mtahiniwa anayeingia katika chumba cha mtihani ndani ya nusu saa ya kuanza kwa mtihani ataruhusiwa kuingia katika chumba cha mkutano, lakini hataongezwa muda wowote kufidia muda aliyochelewa.

2. Watahiniwa watapewa dakika kumi (10) za kusoma maswali kabla ya kuanza kujibu.

3. Msimamizi Mkuu wa mtihani atatoa matangazo yoyote yanayotakiwa kwa watahiniwa kabla ya kuanza kwa mtihani.

4. Bahasha zenye mitihani zilizofungwa na kutiwa lakiri kwa awamu hiyo zitafunguliwa mbele ya watahiniwa.

5. Mtahiniwa yoyote kutokana na sababu yoyote ile ataondoka chumba cha mkutano kwa dharura, atafanya hivyo kwa idhini ya MSIMAMIZI MKUU / MSIMAMIZI MWANDAMIZI na atasindikizwa na MSIMAMIZ MSAIDIZI .

6. Kila mtahiniwa atatakiwa kukaa kwenye dawati lenye namba yake ya mtihani.

7. Bodi haitaruhusu visingizio vyovyote kutoka kwa mtahiniwa atakaye shindwa kutoa kadi ya kitambulisho cha mtihani kinachomruhusu mtahiniwa kuingia kwenye ukumbi wa mtihani,

8. Hakuna mtahiniwa atakayeruhusiwa kuiongia kwneye ukumbi wa mtihani bila ya kuwa na kadi ya kitambulisho cha mtihani alichopewa na barua ya kudahiliwa kwa mtihani.

9. Watahiniwa ni marufuku kuingia kwenye ukumbi wa mtihani, wakibeba au kuwa na aina yoyote ya vitabu na viandikia zaidi ya vile vilivyoruhusiwa na Bodi. Mifuko na mabegi ya mkono n.k ni lazima viachwe mahali palipo bainishwa na msimamizi wa mtihani lakini kuwa tayari kwa lolote litakalotokea.

10. simu za mkononi zisiingizwe kwenye ukumbi wa mtihani kwa sabbu watahiniwa ni marufuku kupiga simu, kupokea simu, kutuma au kupokea ujumbe kwa kutumia nyenzo za simu za mkononi kama vikokotezi au saa wakati mtihani ukiendelea.

11. Mtahiniwa haruhusiwi kuondoa kitabu chake cha kujibia mtihani kuotoka chumba cha mtihani.

12. Mtihiniwa asijihusishe na mwenendo wowote usiokuwa wa kitaalamu uliokusudiwa kumsaidia katika kufanya mtihani.

13. Katika kipindi cha kila somo la mtihani, watahiniwa watatakiwa watie saini kwenye namba zao za mtihani za karatasi ya mahudhurio.

14. Ni jukumu la kila mtahiniwa kudumisha mazingira ya mtihani kwenye ukumbi wa mtihani na kuhakikisha kwamba hatashiriki au kuanzisha mazungumzo yoyote au mwenendo utakaoharibu au kuathiri uzingativu wa watahiniwa wengine wowote .

15. Kila mtahiniwa anatakiwa kuandika Namba ya mtihani kwenye jalada tu. Majina, saini au alama nyingine zozote zitakazoweza kumbainisha mtahiniwa mmoja na mwingine zisiandikwe kwenye jalada la kitabu cha mtihani au karatasi za majibu.

16. Watahiniwa watatakiwa kufuata maelekezo yoyote ya jumla yanayoweza kutolewa na msimamizi Mluu/ Msimamizi Mwanandamizi na kusoma kwa makini maelekezo yaliyoandikwa juu ya karatasi za maswali ya mtihani kama vile yale yanayoonesha idadi ya maswali yanayotakiwa kujibiwa . Zingatia hasa maelekezo yaliyoandikwa kwenye jalada la kitabu cha majibu.

17. Watahiniwa ni marufuku kuvuta, kunywa au kula ndani ya ukumbi wa mtihani.

18. Watahiniwa dakika thelathini kabla ya kumalizika kwa muda wa mtihani wakati msimamizi Mkuu/ Msimamizi mwandamizi atakapotangaza kuwa muda wa mtihani umekwisha, watahiniwa ni lazima waache mara moja kuandika. Maelekezo haya yanatumika si kwa kujibu maswali tu bali pia kwa kujaza hata namba za maswali , vituo na herufi kubwa na uandikaji mwingine wowote.

19. Watahiniwa ni lazima wabaki kwenye viti vyao mpaka msimamizi akusanye vitabu vya majibu kilichotolewa kwa madhumuni hayo kulingana na maelekezo yafuatayo:

 • Jibu la kila swali lazima lianze kwenye ukurasa mpya.
 • Namba ya swali iandikwe juu ya ukurasa kwenye nafasi iliyotolewa.
 • Andika kwenye pande zote za karatasi ya majibu.

 • 20. Majibu yaandikwe kwa wino au kalamu ya ballpen, chati za mtiririko, grafu na na michoro vinaweza kuchorwa kwa penseli.

 • Utaratibu wote wa kujibu maswali ufanywe kwenye kitabu cha majibu.
 • Usichomoe au kuchana karatasi, yoyote kutoka kwenye kitabu cha majibu. Krosi kwa makini kazi yoyote usiyotaka isahihishwe. Usitumie wino wa kufutia maandishi.
 • Iwapo kitabu kikuu cha kuandikia majibu kimetumiwa kwa ukamilifu unaweza kuomba SUPPLEMENTARY ANSWER BOOK ( vitu vya nyongeza).
 • Weka tiki () kwenye maswali yaliyojibiwa ipasavyo.
 • Funga kwa makini vitabu vyovyote vya majibu vya nyongeza na kitabu kikuu cha majibu, na hakikisha kuwa karatasi zote za grafu zimefungwa kwa unadhifu ndani ya kitabu cha majibu na baada ya hapo jaza viboksi kwa usahihi.

 • 21. Majibu yaandikwe kwa muhtasari na kwa mwandiko unaosomeka. Mtindo katika namna ya kuandika majibu utazingatiwa wakati wa kusahihisha kila swali. Watahiniwa wanaonywa kwamba mwenendo wowote wa kutosomeka utawaathiri.

  22. Matumizi ya vidokotezi vya kielekroniki visivyo na sauti, kikotozi telezi na violezi vinaruhusiwa. Watahiniwa ni lazima walete kalamu zao na wanashauriwa kuleta rula pia.

  23. Iwapo kutokana na ugonywa, mtahiniwa atashindwa kuhudhuria mitihani, atamwarifu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi kabla ya kuanza mtihani . Sehemu ya ada inaweza kurudishwa au inaweza kupelekwa mbele kutokana na hiari ya Kamati ya elimu na machapisho. Hakutakiwa ada ya mtihani kwa mtahiniwa anayeahirisha mtihani kutokana na sababu yoyote zaidi ya iliyoelezwa na bodi hapo juu,

  24. Mtahiniwa yoyote utakayeonekana na hatia ya udanganyifu kuhusiana na mtihani au kukiuka sheria na kanuni zozote za mtihani anastahili hatua ya kinidhamu na kuweza kuondolewa kufanya mtihani.

  25. Mwisho wa mtihani , vitabu vya majibu vitakusanywa, kuhakikiwa, kufungashwa na kufungwa, lakini kwa kushuhudiwa na msimamizi mwandamizi , mratibu wa mtihani wa NBAA na mtahiniwa mmoja wa mtihani.

  26. Watahiniwa watafahamishwa matokeo ya mtihani wao mara baada ya Bodi kuwa tayari kufanya hivyo. Matokeo yatawekwa kwenye tovuti ya NBAA na kubandikwa kwenye ubao wa matangazo wa NBAA.