Utafiti

Utafiti ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa. Maarifa mapya na kazi za ubunifu kubadilisha ulimwengu, kujenga mustakabali na kuleta ukuaji endelevu wa taifa. Sehemu ya utafiti ya NBAA ina jukumu la kuratibu utafiti kwa lengo la kusimamia shughuli na mwenendo wa utaalamu zaidi ni kushirikiana na wabia wengine kwenye yanayohusu utafiti.

Vipaumbele vya utafiti

Vipaumbe vya utafiti wa NBAA vinaamuliowa na mahitaji ya mada mahususi na dhamira zinazoonekana na msaada kutoka kwa idara inayohusika na wadau wengine wanaofanyiwa utafiti. Hata hivyo kuna mambo yanayofanya kipaumbele cha utafiti, hayo ni pamoja na:

 • Maagizo ya Bodi ya Utawala
 • Masuala ya Uhasibu ya Taifa yenye maslah kwa umma n.k
 • Mpango wa kitengo cha Utafiti kwa mwaka

Utaratibu wa Utafiti

Kwa kawaida micha kato ya utafiti wa sayansi za jamii au taratibu ni zile zile, tofauti pekee iliyopo inayoweza kuonekana ni mbinu, kwa mtazamo huu, taratibu au michakato ya utafiti wetu inazingatia yafuatayo:-

 • Ubainishaji wa tatizo la utafiti
 • Matayarisho ya mapendekezo ya utafiti yatakayojumuisha yafuatayo

o Usuli/ historia ya tatizo la utafiti
o Malengo
o Uhalali wa utafiti
o Mbinu
o Mpango kazi
o Bajeti ya Utafiti
o Ukusanyaji data
o Uchanganuzi wa data
o Utoaji taarifa

Upangaji Utafiti na mahitaji

Utafiti unafanywa kwa kuzingatia muundo unaoeleweka wa shabaha, majukumu na viashirio, Utaratibu wa karibu wa shughuli za utafiti utawezekana tu iwapo kuna mipango inayoeleweka. Kwa hiyo, upangaji utafiti na mahitaji ya NBAA, ni pamoja na .

 • Kuandaa nyaraka za utafiti na Dodoso na fomu za kukusanyia data, tathimini na takwimu.
 • Kuhudhuria shughuli zote na mawasiliano kuhusu masuala ya utafiti na kudurusu ripoti za utafiti
 • Kutayarisha orodha hakiki ya masuala ya utafiti
 • Kutayarisha mpangoi kazi unaoonesha bajeti
 • Matayarisho ya mahitaji yote kwa ajili ya ziara za ugani yakiwamo mahojianao ya kwenye simu na kupeleka barua
 • Kukudumia mahitaji kwa ajili ya kazi za utafiti.

Machapisho ya Utafiti

Kwa kuwa madhumuni ya utafiti ni kupata maarifa mapya, na kueleza matokeo kwa njia ya machapisho, uhuru wa kuchapisha ni lazima ulindwe kwa nguvu zote. Matokeo ya utafiti uliyofanywa na NBAA yanaweza kupatikana kupitia tovuti ya NBAA majarida ya wahasibu na magazine, Maktaba ya NBAA, na kwa njia nyingine yoyote itakayoonekana kuwa inafaa. (Bofya hapa).