Fellow Certified Public Accountant ( FCPA ) / FCPA-PP

Mtu atastahili kupandishwa hadhi ya usajili kama mhasibu mwanazuoni iwapo ataridhisha Bodi kuwa amekuwa Associate Certificate Public Accountant au Associate Certified Public Accountant katika Public Practice, mwenye rekodi ya uzoefu mzuri wa uytendaji kazi wa miaka saba kabla ya maombi yake kama fellow Certified Public Accountant au Fellow Certified Public Accountant katika Public Practice na ametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taaluma wa uhasibu, ikiwemo

  • Kuwashauri angalau Wahasibu Wahitimu 20 katka kipindi cha miaka saba.
  • Utayarishaji na uwasilishaji wa angalau makala tano kuhusiana na taaluma ya uha sibu katika mkutano wa utunzaji hesabu au ukaguzi
  • Kuchapisha angalau makala tatu kwenye Jarida la Uhasibu la NBAA

Mtu huyo hatimaye anaweza kujaza fomu ya maombi na kuturudishia kwa ajili ya tathimini.